Skip to main content

Licha ya machafuko, amani Masharikiya Kati yaweza kufikiwa: Mladenov

Licha ya machafuko, amani Masharikiya Kati yaweza kufikiwa: Mladenov

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limekutana leo kujadli hali katika ukanda wa Mashariki  ya kati na amani ya  Palestina.

Baraza hilo limesikiliza hotuba iliyotolewa kwa njia ya video kutoka mjini Jerusalem, na Mratibu maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu mchakato wa amani Mashariki ya Kati, Nickolay Mladenov, aliyezungumzia matumaini ya kufikia amani ili kukomesha machafuko zaidi.

Bwana Mladenov  amesema anaamini raia wa nchi hizo hususani Israel na Palestina wanahitaji amani huku akisema bado kuna mivutano na mashambulizi baina ya nchi hizo inayosababisha vifo na majeruhi kadhaa. Hivyo amesema.

(SAUTI MLADENOV)

"Kutokana na kuendelea kwa machafuko, na hali ilivyo sasa, inafanya matazamio ya kurejea katika majadiliano kuwa magumu. Hatua za kijasiri na muhususi lazima zichukuliwe ili kuimarisha maisha. Sitaki kushawishika kuwa Waisrael na Wapalestina wanataka kuishi kwa upanga na katika nchi zenye kuchochea  uhalifu.’’