Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vyoo na huduma za kujisafi ni maendeleo na utu: Ban

Vyoo na huduma za kujisafi ni maendeleo na utu: Ban

Leo ikiwa ni Siku ya Choo Duniani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema huduma za kujisafi ni kiini kwa usafi wa mwanadamu na mazingira, maendeleo pamoja na utu. Taarifa kamili na Amina Hassan.

(TAARIFA YA AMINA HASSAN)

Katika ujumbe wake wa siku hii Bwana Ban amesema licha ya hivyo, kati ya watu watatu duniani , mmoja hapati huduma hiyo na mmoja kati ya wanane hujisaidia hadharani. Hata hivyo amesema ajenda ya maendeleo ya 2030 inatambua umuhimu wa huduma za kujisafi na hivyo kutaka jamii iendelee kuelimishwa na kulindwa dhidi ya hatari ya ukosefu wa huduma za kujisafi ikiwemo vyoo.

Kwa upande wake Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF, limesema kuwa ukosefu wa vyoo unahatarisha maisha ya mamilioni ya watoto maskini zaidi duniani, likionyesha uhusiano kati ya kukosa huduma za kujisafi na utapiamlo.

Watu wapatao milioni 2.4 duniani hawana vyoo, na mtu mmoja kati ya wanane huenda haja kubwa hadharani.

Akizungumzia hali ya huduma za kujisafi na vyoo afisa wa manispaa ya Songea nchini Tanzania Amani Mmasi anasema

(SAUTI MMASI)