Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maandamano COP21 Paris yapigwa marufuku kwa sababu za usalama

Maandamano COP21 Paris yapigwa marufuku kwa sababu za usalama

Ofisi ya Rais nchini Ufaransa, imetoa taarifa kuhusu usalama wakati wa kongamano la Umoja wa Mataifa kuhusu tabianchi jijini Paris, COP21, ikisema kuwa mashambulizi ya kigaidi ya Novemba 13 yamelazimu hatua zaidi zichukuliwe ili kuboresha usalama kwa washiriki wa kongamano hilo, na hivyo kupiga marufuku maandamano yote kuhusu tabianchi. Taarifa kamili na Priscilla Lecomte.

(Taarifa ya Priscilla)

Taarifa hiyo iliyochapishwa kwenye tovuti ya COP21, imesema kuwa serikali ya Ufaransa imeamua kutoruhusu maandamano ya tabianchi yaliyokuwa yamepangwa kufanyika katika mitaa ya Paris na miji mingine nchini Ufaransa mnamo Novemba 29 na Disemba 12.

Hata hivyo, mikutano na matukio mengine yaliyopangwa kufanyika ndani ya kumbi na vyumba mbalimbali yataendelea kama kawaida, kwani usalama katika maeneo hayo unaweza kulindwa kwa urahisi.

Taarifa hiyo imetaja pia mchango wa asasi za kiraia na umuhimu wa kongamano la COP21, ambalo linatarajiwa kuwezesha uchagizaji wa kimataifa na kuchukua hatua kuhusu tabianchi.