Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kampuni za biashara na taasisi 103 zaahidi kuchukua hatua kuhusu tabianchi

Kampuni za biashara na taasisi 103 zaahidi kuchukua hatua kuhusu tabianchi

Zaidi ya kampuni za biashara na taasisi 100 zimetia saini azimio la kuchukua hatua madhubuti za kukabiliana na ongezeko la joto duniani.

Katika azimio hilo lililosainiwa mjini Reykjavík, Iceland, kampuni na taasisi hizo zimeahidi kuchukua hatua za kupunguza uzalishaji wa gesi chafuzi na kupunguza ubadhirifu.

Kulingana na azimio hilo, hatua zinazochukuliwa zitafuatiliwa, na kampuni na taasisi hizo zitachapisha taarifa za mara kwa mara kuhusu hatua hizo.