Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Muziki na hamasisho la uhifadhi mazingira nchini Uganda

Muziki na hamasisho la uhifadhi mazingira nchini Uganda

Kwa kutambua umuhimu wa kulinda mazingira kufuatia mikakati mbali mbali ambayo dunia imechukua kwa ajili ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, wananchi na watu wenye ushawishi katika jamii wanashiriki katika kuhamasisha umma kuhusu ulinzi wa mazingira.

Ni katika muktadha huo  mwanamuziki Austin Danis ameamua kutumia muziki ili kufanikisha lengo hilo nchini Uganda.

Kwa kawaida muziki ambao ni njia ya kupitisha ujumbe na kuelimisha jamii hutumika katika maswala mbali mbali. Je ni vipi muziki unatumika katika kuchagiza ulinzi wa mazingira? Basi ungana na John Kibego katika makala hii.