Skip to main content

MENUB yafunga pazia Burundi

MENUB yafunga pazia Burundi

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kufuatilia uchaguzi nchini Burundi, MENUB umehitimisha rasmi shughuli zake nchini humo kwa hafla iliyofanyika kwenye mji mkuu Bujumbura. Mwandishi wetu wa maziwa makuu Ramadhani Kibuga alikuwa shuhuda wetu.

(Taarifa ya Kibuga)

Sherehe hizo za kuhitimisha kazi za kitengocha Umoja wa Mataifa kilichokuwa kinafuatilia karibu uchaguzi mkuu mwaka 2105 zilihudhuriwa na viongozi mbali mbali na mabolozi wanaowakilisha nchi zao hapa Burundi.

Katika sherehe hizo Tadjoune Diabacte Ali amesoma ujumbe uliowasilishwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon…

(Sauti Tadjoune)

Tunakamilisha kazi za tume ya Umoja wa Mataifa ambayo ilifana, nataka kushukuru serikali na tume ya uchaguzi na kwa wananchi kwa makaribisho waliotupa, hata kama MENUB inafunga milango yake nathibithisha kuwa Umoja wa Mataifa utasalia kusaidia watu na serikali ya Burundi”

Kwa upande wake Issaka Souna kaimu kiongozi katika MENUB ametoa shukrani kwa viongozi wa Burundi na wananchi kwa jumla japo amesema…

(Sauti Issaka)

Tunasikitika kwamba matokeo hayakufikia matarajio yetu lakini, tunajenga matumaini kuwa mazungumzo yatasaidia kumaliza matatizo.”