Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP yaanza kugawa vyakula hospitali, shuleni Ukraine

WFP yaanza kugawa vyakula hospitali, shuleni Ukraine

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP leo limeanza kugawa chakula kwa wagonjwa hospitalini na wanafunzi shuleni katika maeneo yenye mizozo nchini Ukaraine.

Kwa mujibu wa taarifa ya WFP, msaada wa chakula utatolewa kupitia mdau wake wa misaada, shirika la maendeleo na misaada la Adventist ADRA kwa watu takribani 7,000 katika miji kadhaa mashariki mwa taifa hilo la Ulaya lililotatizika kwa mizozo.

Kwa mujibu wa mwakilishi wa ADRA nchini Ukarine Anatoliy Begas, shirika hilo lilitambua kuwa kuongezeka kwa bei za vyakula , kipato kidogo na hali mbaya ya kibinadamu, wagonjwa walioko hospitalini na wanafunzi shuleni huathirika zaidi.

Amesema katika kutekeleza zoezi hilo wanashirikiana na shirika la afya ulimwenguni WHO, na mashirika yaliyoko katika ukanda huo katika kufahamu mahitaji ya raia.