UNESCO kuendesha mjadala maalum kuhusu filosofia

18 Novemba 2015

Likiadhimisha siku ya filosofia duniani, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni(UNESCO), litaendesha majadiliano ya taaluma ya filosofia na kueneza dhana hiyo bila utamaduni wa Magharibi.

Taarifa ya UNESCO inayoangazia mjadala wa siku hiyo utakaourushwa moja kwa moja kupitia mtandao wa intaneti, inasema kuwa filosofia inayovuka mipaka ya utamaduni, kufundisha na kujifunza filosofia katika maeneo na namna mbalimbali ni miongoni mwa mada zitakazojadiliwa.

Kukuza uelewa wa mchango muhimu wa filosofia katika mawazo huru na jukumu lake katika kukuza stahamala na amani, imesema sehemu ya taarifa ya UNESCO.

Shirika hilo limetoa fursa kwa watu kote duniani kushiriki katika mijadala mbalimbali ya siku ya filosofia duniani kwa kutembelea tovuti ifuatayo.

http://www.unesco.org/new/fileadmin/MULTIMEDIA/HQ/SHS/pdf/wpd2015_around...

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter