Skip to main content

Maji ni miongoni mwa sababu kubwa ya majanga duniani : UM

Maji ni miongoni mwa sababu kubwa ya majanga duniani : UM

Maji ni uhai, amekumbusha Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon akihutubia mjadala maalum kuhusu maji na majanga uliofanyika leo kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi.

(Taarifa ya Assumpta)

Bwana Ban amesema kuwapatia raia maji safi na salama ni moja ya majukumu ya msingi ya serikali kote duniani, ili kuhakikishia afya na maendeleo ya jamii.

Amesema ukosefu wa huduma hiyo unaweza kusababisha ukame na njaa, lakini kwa upande mwingine mafuriko yanaweza kusababisha uharibifu mkali na magonjwa, huku akieleleza :

(Sauti ya Ban)

"Mafuriko, ukame na dhoruba yamesababisha asilimia 90 ya majanga 1,000 makali zaidi duniani tangu mwaka 1990. Yamesababisha uharibifu wenye thamani ya dola trilioni moja na kuathiri zaidi ya watu bilioni nne."

Washiriki wa mjadala huo wamezingatia umuhimu wa kutekeleza mfumo wa miaka 15 wa kupunguza hatari za majanga uloafikiwa huko Sendai, nchini Japan mwaka huu, wakisisitiza kwamba kudhibiti majanga kutachangia kukuza maendeleo.