Uwekezaji wa kimataifa ulipanda kwa dola bilioni 441, mwanzoni mwa 2015- UNCTAD

17 Novemba 2015

Miungano na ununuzi wa kampuni wa kuvuka mipaka (M&As) ulishika kasi katika miezi sita ya kwanza ya mwaka 2015, lakini huenda kasi hiyo inapungua mwaka unapokaribia kuisha, kwa mujibu wa ripoti mpya ya Kamati ya Biashara na Maendeleo ya Kimataifa, UNCTAD, kuhusu mwelekeo wa uwekezaji kimataifa.

UNTCAD imesema thamani ya ununuzi wa kampuni ilifika dola bilioni 441 katika miezi sita ya kwanza, ikiwa ni ongezeko la asilimia 136% ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka 2014. Halikadhalika, kiwango hicho ndicho cha juu zaidi tangu nusu ya pili ya mwaka 2007.

Kampuni za kimataifa (MNEs) kutoka nchi zilizoendelea ziliongoza mwelekeo huu wa miungano na ununuzi wa kuvuka mipaka, huku kukiwa na upungufu wa muungano na ununuzi wa kuvuka mipaka kutoka nchi zinazoendelea au chumi zilizoko kwenye mpito.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter