Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Benki ya dunia yaleta nuru kwa wajasiriamali wanawake Ethiopia

Benki ya dunia yaleta nuru kwa wajasiriamali wanawake Ethiopia

Nchini Ethiopia, Benki ya dunia kupitia mfuko wake wa uwezeshaji nchi maskini, IDA imewezesha wanawake zaidi ya Elfu Tatu kujikwamua kiuchumi kutokana na mikopo yenye masharti nafuu.

Miongoni mwao ni Zinabua Hailu ambaye alinzia biashara ya mama ntilie kwa mtaji wa dola 100 akiweka rehani nyumba yao lakini sasa ameweza kupata mkopo wa dola Elfu 38 kupitia IDA.

Bi.Hailu amesema kupitia mkopo huo ameweza kujenga mgahawa na hoteli ya vyumba 10 lakini ndoto yake kuwa kuwa na hoteli kubwa zaidi yenye kiwango cha kimataifa kwa ajili ya watalii.

Francesco Strobbe ambaye ni mchumi wa Benki ya dunia anasema tafiti zinaonyesha kuwa uwezekaji katika biashara zinazoendeshwa na wanawake  zinafursa kubwa zaidi za kuinua vipato katika nchi zinazoibukia kiuchumi.

Amesema hilo ni dhahiri kwa kuwa wajasiriamali wanawake mara nyingi huajiri wanawake wenzao na hivyo ni kichochea katika kupunguza ukosefu wa ajira na kuboresha maisha.