Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tuungane dhidi ya ugaidi na kukuza maendeleo: Ban

Tuungane dhidi ya ugaidi na kukuza maendeleo: Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelihutubia baraza la usalama la Umoja wa Mataifa katika kikao kilichojadili usalama, maendeleo, na vyanzo vya migogoro huku akisema lazima dunia ije pamoja kuviangamiza vikundi vya kigaidi.  Taarifa an Assumpta Massoi.

(TAARIFA YA ASSMUPTA)

Bwana Ban amesema katika kutekeleza hilo ni muhimu kuhuisha uwezo wa kutuma vikundi kwa ajili ya kusaidia mamlaka za kitaifa kabla ya kuanza kwa migogoro, kuweka uwazi zaidi katika kuhusisha mamlaka za kitaifa na nchi wanachama.

(SAUTI BAN)

‘‘Juhudi zimesongeshwa. Mfumo wa tahadhari mapema na kuwajibika haraka umeimarishwa. Katika baadhi ya matukio,  kuweka mbele haki za binadamu kuwewezesha Umoja wa  Mataifa kushughulikia tahadhari za mapema haraka na kwa ufanisi kuliko awali.’’

Kuhusu maendeleo Katibu mkuu ameliambia baraza la usalama kuwa maendeleo ambayo huacha watu nyuma hupanda mbegu ya machafuko na ukosefu wa uendelevu akisisistiza kuwa ajenda ya maendeleo ya mwaka 2030 lazima iwe sehemu kubwa ya mkakati wa kimaendeleo.

Mkutano huo pi aumehudhuriwa na wawakilishi wa asasi nne za za kiraia zilizoshinda tuzo ya amani ya Nobel nchini Tunisia kutokana na mchango wao katika ujenzi wa  demokrasia.