Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza laridhia kikosi cha dharura, RRF huko CAR

Baraza laridhia kikosi cha dharura, RRF huko CAR

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeridhia ombi la kupelekwa kwa kikosi cha dharura cha kuchukua hatua huko Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, kufuatia ongezeko la mapigano ya kikabila na ukatili wa kingono nchini humo.

Naibu mwakilishi wa Uingereza kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Peter Wilson ambaye nchi yake inashika urais wa Baraza la Usalama kwa mwezi huu, amesema hayo alipozungumza na waandishi wa habari baada ya kikao cha faragha kuhusu CAR.

Katika kikao hicho, walipokea taarifa kutoka kwa mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa na Mkuu ofisi ya umoja huo inayoratibu masuala ya kibinadamu ambapo kwa ujumla walielezea kuzidizi kuzorota kwa usalama na maisha ya raia yakizidi kuwa hatarini.

(Sauti ya Balozi Wilson)

Kutokana na ongezeko la ghasia, Baraza la usalama limeridhia ombi  la kupelekwa kwa muda huko CAR kikosi cha dharura cha kuchukua hatua kutoka UNOCI. Tutatoa taarifa rasmi siku zijazo.”

Hata hivyo amesema wanaendelea kusaka kuwepo kwa suluhu ya muda mrefu katika ghasia za sasa zinazoendelea na kwamba..

(Sauti ya Balozi Wilson)

Halikadhalika tunatumia kuwa kwa kupeleka walinda amani zaidi kusaidia ujumbe wetu na pia kuimarisha ulinzi kuelekea ziara ya Pope mwishoni mwa mwezi Novemba, hii itasaidia kulinda raia. Na pia kwa uwepo wa Pope kusaidia kuimarisha na kuchagiza mashauriano na maridhiano kabla ya uchaguzi mwishoni mwa mwaka huu.”