Elimu na Utamaduni mbinu za kupambana na itikadi kali : UNESCO
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi, na Utamaduni UNESCO, Irina Bokova, amesema leo ni jukumu la kila mtu kupambana na itikadi kali, kwa kukuza haki za binadamu na elimu kwa wote.
Amesema hayo akizundua mkutano wa viongozi, mjini Paris, Ufaransa, leo ikiwa ni miaka 70 tangu kuanzishwa kwa shirika hilo.
Pamoja na kauli hiyo, Bi Bokova pia amekikariri salamu zake za rambirambi kwa wahanga wa mashambulizi ya kigaidi yaliyotokea tarehe 13 Novemba, mjini Paris, Ufaransa, akisema vitendo hivyo ni uhalifu dhidi ya uhuru, stahamala na ubinadamu kwa ujumla.
Amesema ili kupambana na ugaidi, ni lazima kutumia mbinu zisizo kali kama vile elimu au sayansi, huku akitaja mistari ya kwanza ya mkataba wa UNESCO :
(Sauti ya Bi Bokova)
"Kwa kuwa vita vinaanza kwenye vichwa vya watu, ni kwenye fikra hizo zenye vita ambapo ni lazima kujenga ulinzi wa amani. Hii ni nguzo ya shirika letu, na hii imefaa zaidi siku kama leo na imekuwa na dharura na umuhimu zaidi. "