Baraza la haki za binadamu laangaziwa Baraza Kuu

Baraza la haki za binadamu laangaziwa Baraza Kuu

Baraza la Haki za binadamu la Umoja wa Mataifa likiwa linakaribia kutimiza muongo mmoja tangu kuanzishwa kwake, bado ulimwengu umesalia kuwa na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.

Amesema Joachim Rücke, Rais wa baraza hilo wakati akiwasilisha ripoti ya mwaka ya baraza lake mbele ya baraza kuu la Umoja wa Mataifa akitaja Syria kuwa ni moja ya nchi ambazo suala lake lilishika ajenda ya juu kutokana na mzozo wake ulioingia mwaka wa tano…

(Sauti ya Rücke)

Na mamlaka ya kamisheni yake ya  uchunguzi iliongezwa kwa mara nyingine. Kamisheni hiyo mwezi Septemba iliwasilisha ripoti yake ya 10, ambayo inaweka bayana vitendo vya ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu kwa mapana yake.”

Amegusia pia vitisho wanavyopata watetezi wa  haki za binadamu na wanarahakati ambao amesema wana jukumu kubwa kusaidia  kazi za Baraza hilo..

(Sauti ya Rücke)

“Na kwamba bila mchango wa taasisi za kiraia, kazi za baraza, tathmini za mwaka na shughuli nyingine hazitakuwa thabiti. Ushiriki wao lazima uzingatiwe na wahusika wasipate vitisho  vyovyote.”