Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ki-moon aomba kuchukua fursa ya kiplomasia kusitisha mzozo Syria

Ban ki-moon aomba kuchukua fursa ya kiplomasia kusitisha mzozo Syria

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema leo kwamba ametiwa moyo na mkutano wa wadau wa kimataifa mjini Vienna ili kutatua mzozo wa Syria na kupata suluhu ya kisiasa haraka iwezekanavyo.

Kwenye taarifa iliyotolewa na msemaji wake, Bwana Ban amenukuliwa akieleza matumaini yake kuhusu matokeo ya mkutano ili kufikia sitisho la mapigano na kuhakikisha ufikishaji wa misaada ya kibinadamu.

Katibu Mkuu amekariri pia uungaji mkono wa Umoja wa Mataifa katika utaratibu huo, huku akiwaomba wadau kuchukua fursa hiyo ya kidiplomasia ili kupata suluhu ya kisiasa.

Kwa upande wake Mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Syria Staffan de Mistura amesema kwamba bado yuko tayari kuitisha mazungumzo ya kisiasa baina ya wadau wa Syria.