Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

El-nino ikitarajiwa, WHO yasaidia kutokomeza kipindupindu Tanzania

El-nino ikitarajiwa, WHO yasaidia kutokomeza kipindupindu Tanzania

Mvua za  el-nino zikakribia katika ukanda wa Afrika Mashariki, serikali ya Tanzania imejizatiti kukabiliana na ugonjwa wa kipindupindu ambao unakabili mikoa 17 ya nchi hiyo.

Shirika la afya ulimwenguni WHO kwa kushirikiana na wadau linaratibu masuala ya kiufundi, madawa na mambo mengineyo ili kuhakikisha ugonjwa huo uliogarimu maisha ya zaidi ya watu 100 na kuathiri wengine zaidi ya 8,000 unatoweka.

Katika mahojano na Joseph Msami wa idhaa hii, Msaidizi wa kitengo cha udhibiti wa magonjwa ya mlipuko kwenye wizara ya afya nchini Tanzania, Dkt. Janeth Mghamba anaeleza hatua za kukakibili kipindupindu akianza na hali ya maambukizi kwa sasa.