Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwai Kibaki ateuliwa Mjumbe Maalum wa UNESCO barani Afrika

Mwai Kibaki ateuliwa Mjumbe Maalum wa UNESCO barani Afrika

Rais Mstaafu wa Kenya Mwai Kibaki ameteuliwa kuwa Mjumbe Maalum wa masuala ya maji wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO.

Uteuzi huo umefanywa na Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Irina Bokova ambapo kwa mujibu wa ttaarifa iliyotolewa leo na UNESCO, uteuzi huo unatambua mchango mkubwa wa rais huyo mstaafu katika kuelimisha jamii kuhusu matumizi endelevu ya maji na kufikisha huduma za maji kwenye sehemu zote.

Maadhimisho ya uteuzi rasmi yatafanyika tarehe 17, Novemba, mjini Paris Ufaransa.

Mwai Kibaki amekuwa Rais wa Kenya kuanzia Disemba 2002 hadi April mwaka 2013.

Ameanzisha taasisi yenye jina lake kwa ajili ya kukuza nishati rafiki kwa mazingira, diplomasia ya maji na kuendeleza kilimo cha kahawa.

Pia amekuwa mhisani wa Shirika la Millenium Water Alliance lenye lengo la kuhakikishia huduma za maji kwenye jamii zinazokumbwa na upungufu wa maji.