Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Siku ya Afya Duniani itamulika ugonjwa wa kisukari- WHO

Siku ya Afya Duniani itamulika ugonjwa wa kisukari- WHO

Kuelelekea Siku ya Kisukari Duniani hapo kesho Novemba 14, Shirika la Afya Duniani, WHO, limetoa wito hatua zaidi zichukuliwe ili kubadili mwelekeo wa wimbi linaloongezeka la ugonjwa wa kisukari duniani, huku ikitangaza kuwa Siku ya Afya Duniani Aprili Saba mwakani itaangazia suala la ugonjwa huo wa kisukari.

WHO imesema Siku ya Afya Duniani itatoa jukwaa muhimu la kupigia chepuo juhudi za kuzuia kisukari na kuhakikisha kuwa ugonjwa huo unaojitokeza kwa aina tofauti unadhibitiwa ipasavyo miongoni mwa watu wanaoishi nao.

Aidha, Shirika hilo limetaja baadhi ya hatua zinazoweza kuchukuliwa ili kupunguza athari za kisukari, zikiwemo kushiriki mazoezi ya mwili na kuzingatia mlo wenye afya, pamoja na hatua za serikali kama vile kudhibiti matangazo ya bidhaa za vyakula vinavyodhuru afya, na kuhakikisha kuwa mifumo ya afya inatoa huduma zinazohitajika na watu wanaoishi na kisukari.

Dkt. Nasoro Mouhamed ni mtaalam wa ugonjwa wa kisukari nchini Burundi.

(Sauti ya Dkt. Mouhamed)