Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Shindano la uandishi wa habari za ukeketeji; muda bado: UNFPA

Shindano la uandishi wa habari za ukeketeji; muda bado: UNFPA

Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu UNFPA limeanzisha tuzo ya uandishi wa habari kuhusu ukeketaji Afrika

Tuzo hiyo iliyoanzishwa kwa ushirikiano na gazeti la Uingereza la The Guardian inatarajia kuimarisha uelewa kuhusu ukeketaji na kutambua jitihada za waandishi wa habari katika hilo.

Mshindi wa tuzo hiyo atapewa masomo ya mwezi mmoja kwenye idara ya ukeketaji ya the Guardian, akilipiwa safari na matumizi yake yote kule London.

Ili kushiriki mashindano hayo, mtu anapaswa kuwa raia wa nchi iliyoko barani Afrika, na awe mwandishi wa habari anayefanya kazi kwenye gazeti, radio au televisheni iliyopo Afrika.

Anapaswa kutuma kabla tarehe Nne Januari mwaka 2016 ripoti yake ya maneno yasiyozidi 2,000 au makala ya redio au televisheni yenye muda wa kati ya dakika Nne hadi 15 kuhusu ukeketaji, iliyotangazwa mwaka huu wa 2015.

Maelezo zaidi kuhusu tuzo hiyo yanapatikana kwenye tovuti ya UNFPA.