Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sanaa ya maigizo yatumika kutokomeza Ebola Sierra Leone.

Sanaa ya maigizo yatumika kutokomeza Ebola Sierra Leone.

Ugonjwa wa Ebola ulitikisa Sierra Leone kwa muda zaidi ya mwaka mmoja na kugarimu maisha ya zaidi ya watu 3,000. Shirika la Afya Duniani, WHO linasema sasa nchi hiyo imejikomboa na ugonjwa huu hatari, na kuipongeza serikali na wananchi kwa kufanya kazi kwa bidii na kujitolea wakati wakipambana na kuibuka zaidi kwa Ebola katika historia ya binadamu.

Shirika la Kuhudumia Watoto, UNICEF na WHO pamoja na wadau wengine wanafanya nini ili kuhakikisha ugonjwa huu unakoma nchini humo? Ungana na Amina Hassan katika makala itakayosafirisha hisia zako hadi nchini humo.