Haki za watu wa asili Honduras mashakani: Mtaalamu

12 Novemba 2015

Mtaalamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu, Victoria Tauli-Corpuz ameonya kuhusu ukiukaji wa haki za ardhi na maliasili za watu wa asili kando ya kukosa huduma za afya, elimu na sheria nchini Honduras. Maelezo zaidi na John Kibego.

Baada ya ziara yake ya siku 9 nchini Honduras Bi. Tauli-Compuz  amesema, tatizo la msingi linalowakabili ni kutotanbuliwa kikamlifu, kutopewa ulinzi na haki kwa ardhi za mababu zao na maliasili.

Aidha, ameonyeshwa kusikitishwa na mazingira ya ukatili kwa ujumla dhidi jamii nyingi za watu wa asili nchini humo.

Mtaalam huyo ambaye alishuhudia mazingira ya jamii za Auka na Miskito  miongoni mwa nyingine, ameitaka serikali ya Honduras kuchunguza na kuwashitaki wale wote waliohusika na uuzaji wa ardhi na uchafuzi wa mazingira kama ilivyoafikiwa katika mkataba na jamii, ili wakamilishe mchakato wa kuwarejesha kwenye ardhi zao.

Nayo jamii ya Lenca iliyopinga mradi wa Bwawa la Umeme kwa kuhofia athari zake kwa maisha yao, walimweleza Bi. Sauli-Compuz kuwa wanakabiliwa na vitisho na mauaji.