Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mafunzo ya UNESCO yanalenga kuhakisha maendelo ya kiteknolojia kwa wanafunzi wenye ulemavu, Kenya

Mafunzo ya UNESCO yanalenga kuhakisha maendelo ya kiteknolojia kwa wanafunzi wenye ulemavu, Kenya

Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni, UNESCO linaendesha warsha maalum kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa washikadau mbali mbali wa sekta ya elimu nchini Kenya kwa lengo la kuboresha mifumo ya kidijitali kwa wanafunzi walio na ulemavu.

Warsha hiyo ya siku tano kuanzia Novemba 9 hadi 13 inayofanyika mjii mkuu wa Kenya,Nairobi ni kwa ushirikiano wa UNESCO na  serikali ya Kenya.

Katika mahojiano na Grace Kaneiya wa Idhaa hii msaidizi katika kitengo cha habari na mawasiliano UNESCO, Kenya Shaylor Mwanje amezungumzia umuhimu wa mafunzo hayo hapa anaanza kwa kuelezea lengo lake.