Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chapa na umuhimu wake katika soko na ushindani wa kibiashara:WIPO

Chapa na umuhimu wake katika soko na ushindani wa kibiashara:WIPO

Makampuni kote duniani yametumia  kiasi cha  dola nusu trilioni kwa mwaka katika chapa za bidhaa,  kiasi kikubwa cha fedha hizo kikitumia katika utafiti na ubunifu limesema shirika la kimataifa la hakimili WIPO.

Hii ni kwa mujibu wa ripoti ya pili ya WIPO kuhusu hakimiliki duniani iliyopewa kichwa hadhi na sura katika soko la kimataifa, inayotoa taarifa na uchambuzi kuhusu namna  makampuni yanatumia chapa katika kutofautisha bidhaa zao dhidi ya mahasimu kibiashara na ukuaji wa matumizi ya chapa na maana yake kwa mteja katika muktadha wa soko, ushindani na ubunifu.

Afrika Mashariki hususani Tanzania WIPO imetumia mfano wa kampuni iitwayo Azam kudhihirisha ukweli wa umuhimu wa chapa katika soko na ushindani kama inavyoainisha ripoti hiyo. Ungana na Asumpta Massoi katika makala yenya ufafanuzi zaidi.