Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Japan na Marekani zaongoza katika uvumbuzi wa teknolojia za kisasa:WIPO

Japan na Marekani zaongoza katika uvumbuzi wa teknolojia za kisasa:WIPO

Ripoti mpya ya shirika la hakimiliki duniani, WIPO inaonyesha kuwa Japan na Marekani zinaongoza katika orodha ya nchi chache duniani zinazochochea uvumbuzi wa teknolojia za kisasa.

Teknolojia hizo ni pamoja na zile za uchapishaji wa nyaraka katika pande tatu 3D, utengenezaji wa roboti na teknolojia ya Nano, teknolojia ambazo WIPO imesema zinaweza kuchochea ukuaji mkubwa wa kiuchumi duniani na kubadili maisha ya wakazi wa sayari ya dunia.

Mkurugenzi Mkuu wa WIPO Francis Gurry ametolea mfano ugunduzi wa ndege, antibayotiki na vipitisha umeme, akisema ulileta mabadiliko makubwa na kuchochea biashara kwa mantiki hiyo amesema anataja mambo muhimu yaliyopatiwa msisitizo na ripoti hiyo..

(Sauti ya Gurry)

“Mosi inasisitiza kwa mara nyingine tena misingi ya uvumbuzi kuwa ni serikali kupatia fedha utafiti wa kisayansi na kuweka mazingira rafiki ya kuzitoa teknolojia hizo kwenye maabara ili zitengezwe kwa matumizi.Pili soko lenye ushindani linalochochea kampuni kufanya uvumbuzi huku zikiungwa mkono na soko la fedha na sera nzuri. Na tatu ni uhusiano kati ya wavumbuzi katika sekta ya umma na ile binafsi.”

Japan, Marekani, Ujerumani, Ufaransa, Uingereza na Jamhuri ya Korea zinamiliki asilimia 75 au zaidi ya maombi ya haki za hataza kwenye nyanja ya uchapishaji wa picha za pande tatu, teknolojia Nano na roboti.

Teknolojia ya Nano inasaidia wanasayansi katika nyanja kadhaa ikiwemo kuongeza kasi ya mawasiliano kwenye simu na hata utakasishaji wa maji viwandani.