Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wataalam wa UM wakaribisha kuachiwa huru kwa mwandishi wa habari Misri

Wataalam wa UM wakaribisha kuachiwa huru kwa mwandishi wa habari Misri

Mtaalamu maalum wa Umoja wa MatAifa kuhusu uhuru wa kujieleza David Kaye na yule wa Watetezi wa Haki za Binadamu, Michel Forst,  wamefurahia kuachiliwa huru kwa mwanahabari wa Misri, Hossam Bahgat ambaye amekuwa kizuizini tangu 8. Novemba.

Wakikaribisha hatua hiyo, wajumbe hao maalum wa Umoja wa Matifa,  wamelezea kuguswa na vitisho dhidi ya wanahabari na watetezi wa haki za binadamu nchini Misri ambavyo vinakandamiza haki zao na kudidimiza utendaji kazi.

Mjumbe David Kaye amesema kuzuilwa na hatimaye kuachiliwa hurukwa Hossam Bahgat, kunatoa ujumbe wa kukiukwa kwa kanuni za kulinda uhuru wa kujieleza ambazo Rais Fata Al-Sisi alitoa hivi karibuni na kuahihidi kuwa serikali yake itazitii.

Naye Mjumbe Maalum kuhusu Hali ya Wateteezi wa Haki za Binadamu, Michael Forst amesema kisa hiki kimeshuhudiwa wakati ripoti zinazoaminika zikisema wanahabari kadhaa wanazuiliwa na mamlaka za Misri.

Hossam Bahgat, aayejulikana sana nchni humo kwa kuandika ripoti za uchunguzi kuhusu haki za binadamu anaaminika kukamatwa katika uchunguzi uliyofanywa na wanajeshi kuhusiana na ripoti zake.