Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mvua za masika fursa ya nzige kuibuka:FAO

Mvua za masika fursa ya nzige kuibuka:FAO

Shirika la chakula na kilimo duniani, FAO limeonya kuwa mvua kubwa zilizonyesha hivi karibuni katika ukanda wa kaskazini-magharibi mwa Afrika pamoja na vimbunga mfululizo huko Yemen zimeweka mazingira ya kuibua kuibuka kwa nzige ambao ni hatari kwa uharibifu wa mazao. John Kibego na maelezo zaidi.

(Taarifa ya Kibego)

Mtaalamu wa FAO kuhusu masuala ya nzige, Keith Cressman amesema mvua kubwa husababisha udongo kuwa na unyevunyevu na wadudu kuweza kutaga mayai yao na hivyo baa la nzige linaweza kuharibu mazao na wanyama na kutishia uhakika wa chakula na kipato vijijini.

Kwa mantiki hiyo amesema wakati mvua za El Nino nazo zikitarajiwa kuendelea, ni vyema nchi zikachukua hatua baada ya mvua kufuatilia kwa miezi sita ili kuchukua hatua sahihi ikiwemo kudhibiti mazalia na kusambaa kwa nzige.

Kwa mujibu wa FAO kwa siku moja tu kundi dogo la nzige linaweza kuharibu mazao ya chakula yanayoweza kutumika kukidhi watu elfu 35.