OCHA, WFP , Ethiopia kuukabili ukame

10 Novemba 2015

Timu ya usaidizi wa kibinadamu nchini Ethiopia imetangaza keo kwamba inaratibu ukusanyaji wa misaada kwa ajili ya watu milioni 8.2 wanaohitaji usaidizi wa dharura nchini humo kutokana na ukame.

Taarifa iliyotolewa leo imeekeza kwamba mvua zimeadimika tangu mwanzo wa mwaka na hivyo kusababisha ukame mkali, ukosefu wa maji na utapiamlo kwenye baadhi ya maeneo ya nchi.

Mkuu wa ofisi ya kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA nchini humo Paul Handley ameipongeza serikali ya Ethiopia kwa jitihada zake katika kuandaa usaidizi wa dharura, tayari ikiwa imekusanya dola milioni 200 kwa ajili ya kusaidia wafugaji na kutoa huduma za maji.

Kwa upande wake mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula WFP nchini humo amesema uongozi bora wa Ethiopia utaisaidia nchi kukabiliana na changamoto hiyo bila kurudi nyuma kimaendeleo.

Hata hivyo, taarifa imesisitiza kwamba usaidizi wa kimataifa unahitajika ili kutimiza mahitaji ya fedha katika swala hilo.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter