Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

El Nino yahatarisha maisha ya watoto Afrika

El Nino yahatarisha maisha ya watoto Afrika

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEf limekadiria kwamba watoto milioni 11 wanaweza kuathirika kwa njaa, magonjwa na ukosefu wa maji kwenye maeneo ya Afrika Mashariki na Kusini kutokana na kuongezeka kwa mvua na ukame zilizosababishwa na El nino.

Akizungumza leo na waandishi wa habari mjini Geneva Uswisi, msemaji wa UNICEF Christophe Boulierac amesema kwamba magonjwa yanayoweza kuathiri watoto ni malaria, homa ya denge, kuhara na kipindupindu.

(Sauti ya Bwana Boulierac)

“ Hali ya hewa mbaya zaidi iliharibu riziki ya jamii, watoto wadogo mara nyingi huathiriwa na utapiamlo, na wanakuwa hatarini zaidi kuugua, kuchelewa kukua kiakili na kufariki dunia mapema.”

Miongoni mwa nchi zilizoathirika na El Nino ni Somalia ambayo imekumbwa na mafuriko, na Ethiopia ambayo inakabiliwa na ukame mbaya zaidi kwa kipindi cha miaka 30.