Shule za jamii zaelimisha watoto ukimbizini

Shule za jamii zaelimisha watoto ukimbizini

Vita vinavyoikumba Syria vimesababisha mamilioni ya watu kukimbia makwao na watoto wengi kuacha shule. Nchini Lebanon ambako kuna zaidi ya wakimbizi Milioni Moja wa Syria, mashirika ya kibinadamu yanahaha kutoa huduma za elimu kwa watoto wasyria 400,000 wenye umri wa kuandikishwa shuleni.

Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR, nusu ya watoto hao hawana nafasi kwenye shule zilizoandaliwa na mashirika hayo.

Ili kukabiliana na changamoto hiyo, jamii inajitahidi kupata suluhu kuwaelimisha watoto waliopo kambini, kama anavyoeleza Priscilla Lecomte kwenye makala hii.