Ban awapongeza Wamyanmar kwa uchaguzi, awasihi kudumisha utulivu

Ban awapongeza Wamyanmar kwa uchaguzi, awasihi kudumisha utulivu

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amewapongeza watu wa Myanmar kwa subira, utu na hamasa waliyoonyesha wakishiriki uchaguzi wa Jumapili Novemba 8, 2015.

Bwana Ban ameipongeza kamisheni ya muungano ya uchaguzi na taasisi nyingine za kitaifa na mikoa kwa kazi zinazofanya.

Wakati matokeo ya uchaguzi yakianza kuwasilishwa, Katibu Mkuu amewasihi wadau wote nchini Myanmar kuendeleza moyo wa utu, utulivu na heshima katika kuhitimisha mchakato wa uchaguzi.