Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ampongeza Amina Mohamed kuteuliwa waziri Nigeria

Ban ampongeza Amina Mohamed kuteuliwa waziri Nigeria

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amempongeza msadizi wake aliye pia mshauri wake maalum kuhusu mipango ya maendeleo baada ya 2015 Bi Amina J. Mohamed kwa kuteuliwa katika baraza la wamwaziri nchini mwake Nigeria.

Taarifa ya Katibu Mkuu kupitia ofisi ya msemaji wake inasema kuwa Ban amemshukuru kwa huduma yake katika kuandaa agenda ya maendeleo ya 2030.

Amesema licha ya kuwa ulikuwa ni mwaka wa majadiliano magumu na mchakato wa mashauriano jumuishi katika historia ya Umoja wa Mataifa, maono yake na sauti vilisaidia kuwaleta watu pamoja na kufikia makubaliano kimataifa kuhusu maendeleo enedelevu, SDGS.