Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwaka 2016 ni muhimu kwa Somalia: Hammond

Mwaka 2016 ni muhimu kwa Somalia: Hammond

Uingereza imesema mwaka ujao wa 2016 utakuwa ni muhimu sana kwa Somalia kudhihirisha kuwa inajikwamua kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Kaulil hiyo ametoa Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza Phillip Hammond alipozungumza na waandishi wa habari baada ya kuongoza mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu Somalia, uliopitisha azimio la kuimarisha uwepo wa umoja huo nchini humo.

Bwana Hammond amesema..

(Sauti ya Hammond)

“Mwaka ambao jamii ya kimataifa inataka kuona chaguzi halali, mwaka ambao serikali ya shirikisho itadhiisha ina uwezo wa kuweka na kuandaa na kusimamia bajeti na kuendesha serikali katika mazingira ambayo yataruhusu taasisi za kifedha za kimataifa kushirkiana na nchi na kuweka mipango ya usaidizi. Na pia ni mwaka ambao serikali ya shirikisho itadhihirisha kuwa marekebisho ya jeshi la kitaifa yatawezesha liwe na uwezo na lichukue majukumu yanayofanywa na AMISOM.”

Kwa mantiki hiyo akatoa hakikisho la nchi  yake kwa Somalia.

(Sauti ya Hammond)

“Uingereza itandelea kushirikiana na Somalia kufanikisha ajenda hizo na kukabili changamoto na ninafurahi kuwa leo asubuhi tumepitisha kwa kauli moja azimio la baraza la usalama la Umoja wa Mataifa linalopendekeza usaidizi zaidi kwa azma hiyo.”

Waandishi wa habari wakauliza kuhusu Al Shabaab kuchochea misimamo mikali miongoni wma vijana ili kutikisa serikali ambapo Waziri Hammond amesema kadri serikali inavyozidi kuimarika..

(Sauti ya Hammond)

“Itakuwa inaangalia sambamba na programu ya ulinzi, kuweka programu ya kuondoa harakati za kuchochea misimamo mikali pamoja na ugaidi. Na tutakuwa tayari kusaidia wanavyofanya hivyo.”

Uingereza ndiyo inashikilia kiti cha urais wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa mwezi huu wa  Novemba.