Polio yasalia hatari kubwa Sudan

Polio yasalia hatari kubwa Sudan

Watoto Milioni 4 wenye umri wa chini ya miaka mitano wamepewa chanjo dhidi ya polio katika kampeni ya kitaifa ya chanjo iliyokamilika wiki iliyopita nchini Sudan.

Serikali ya Sudan imekamilisha zoezi hilo kwa ushirikiano na shirika la afya duniani, WHO, shirika hilo likisema kwenye taarifa yake ya leo kwamba Sudan iko hatarini sana kuathirika na mlipuko wa polio kwa sababu ya idadi kubwa ya wakimbizi wa ndani nchini humo.

Kwa mujibu wa WHO, watoto 162,000 wenye umri wa chini ya miaka mitano hawafikishwi na timu zinazotoa chanjo kwenye maeneo yaliyokumbwa na machafuko.

WHO inashirikiana na Wizara ya Afya ili kuijengea uwezo wa kifedha na kitaaluma katika kufikia watu hao wote na kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa chanjo.