Ubunifu watumiwa kwa ajili ya watoto: UNICEF
Kongamano la Ubunifu limezinduliwa leo mjini Helsinki, nchini Finland ambapo watalaam wa teknolojia mpya wanakutana kujadili jinsi ya kutumia ubunifu kwa ajili ya kusaidia watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu zaidi. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi.
(Taarifa ya Assumpta)
Kongamano hilo liitwalo “Start Up to Scale Up” limeandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Finland na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF.
Lengo ni kuongeza uelewa kuhusu faida za ubunifu kwa watoto, kuunda ubia mpya kwa ajili ya kukuza suluhu bunifu, kusaka ushirikiano wa wadau mbali mbali na kuandaa ubunifu mpya ili kutokomeza umaskini wa watoto.
Miongoni mwa mada zitakazojadiliwa ni takwimu za kijamii, upatikanaji wa habari kupitia setilaiti, faida ya michezo na teknolojia za masomo katika kukuza ubunifu.