Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mvua za El-Nino zatarajiwa Afrika Mashariki: UNISDR

Mvua za El-Nino zatarajiwa Afrika Mashariki: UNISDR

Wakati ambapo eneo la  mashariki ya kati linakumbwa na dhoruba kali, ukanda wa Afrika Mashariki pia unakabiliwa na mvua nyingi, watalaam wakielezea kwamba hizo zimesababishwa na mabadiliko ya tabianchi ambayo husababisha halijoto ya maji ya bahari ya Pacifiki kupanda na mfumo wa mvua kubadilika kabisa duniani kote, tukio hili likijulikana kwa jina la El Nino.

Tayari mwaka 1998 El Nino iliathiri ukanda wa Afrika Mashariki kupitia mvua kali na hatimaye ukame wa kihistoria uliosababisha madhara makubwa. Kupitia ofisi yake ya kikanda, Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na kupunguza madhara ya majanga UNISDR inashirikiana na serikali za nchi za Afrika Mashariki ili kuimarisha uelewa na utayarishaji wa jamii kukabiliana na hali hiyo.

Julius Kabubi ni mtalaam wa UNISDR - Nairobi, Kenya na anamwelezea Priscilla Lecomte hali iliyvo sasa kwenye ukanda huo.