Hakuna tena Ebola Sierra Leone:WHO

7 Novemba 2015

Shirika la afya ulimwenguni WHO leo limetangaza kuwa hakuna tena mlipuko wa homa kali ya Ebola nchini Sierra Leone.

Hii inafuatia siku mbili za kutokuwepo kwa kisa chochote cha Ebola na hivyo kufanya mfululizo wa majuma saba bila kisa kipya.

Mwakilishi wa WHO nchini Sierra Leone  Dk Dr Anders Nordström amesema tangu kuripotiwa kwa kisa cha kwanza mwezi Mei mwaka 2014, watu zaidi ya elfu nane waliathiriwa, zaidi ya elfu tatu kufariki, 221 kati yao wakiwa ni wahudumu wa afya na kuongeza kuwa leo ni kumbukumbu ya wote waliofariki.

Amesema nchi hiyo itakuwa chini ya ufuatiliaji maalum hadi Februari tano mwakani na WHO itaendelea kusaidia katika wakati huo. Dk Nordström ameongeza kuwa awamu hiyo ya uangalizi na ufauatiliaji ni muhimu katika kuhakikisha utambuzi wa uwezekano wa kisa chochote cha Ebola.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud