Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Harakati za kuhifadhi muziki wa asili nchini Iran

Harakati za kuhifadhi muziki wa asili nchini Iran

Utamaduni ni jambo linalotambulisha jamii ya eneo fulani kwa wakati fulani. Kadri siku zinavyoenda, tamaduni ambazo zimekuwa zinatambulisha jamii fulani ziko hatarini kutoweka kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo utandawazi na ukosefu wa juhudi za kuhifadhi tamaduni hizo. Ni kwa mantiki hiyo shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO lina jukumu la kuhifadhi mali hizo adimu na miongoni mwao ni utamaduni wa muziki wa kiasili wa huko Iran, ukibeba utamaduni wa kiajemi. Muziki huo wa karne na karne zilizopita ni wa kiwango cha juu na umeorodheshwa kwenye urithi wa utamaduni wa binadamu.

Je ni wa aina gani? Ungana na Assumpta Massoi kwenye makala hii.