Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kimbunga kipya Megh chajikusanya kukumba Yemen

Kimbunga kipya Megh chajikusanya kukumba Yemen

Wakati harakati za uokozi dhidi ya kimbunga Chapala zikiendelea nchini Yemen, Kimbunga kipya kiitwacho Megh kinajikusanya kutokea bahari ya Uarabuni kuelekea kulikumba eneo hilo. Grace Kaneiya na maelezo kamili

(TAARIFA YA GRACE)

Kwa mujibu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya usaidizi wa kibinadamu OCHA, kimbunga Megh kinatarajiwa kuikumba Yemen mnamo jumapili ya Novemba nane ambapo jumuiya ya misaada ya kibinadamu inafuatailia kwa karibu tishio hilo.

OCHA imesema kwamba imejipanga kukabiliana na athari za kimbunga hicho wakati huu ambapo kile cha awali yaani Chapala kimesababisha vifo vya watu wanane, wakiwamo watoto wawili na kujeruhi zaidi watu 30.

Chapala pia kinatwajwa kusababisha mafuriko makubwa na uharibifu wa mali na mazao husasani Kusini Mashariki mwa Yemen.