Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mjadala waibuka kuhusu masafa kwa ajili ya ndege zisizo na rubani

Mjadala waibuka kuhusu masafa kwa ajili ya ndege zisizo na rubani

Mkutano kuhusu mawasiliano ya radio duniani umeingia siku ya Tano hii leo huko Geneva, Uswisi ambako majadiliano yanaendelea kuhusu mgao wa masafa huku tofauti za maendeleo ulimwenguni zikiibua mjadala juu ya aina ya matumizi ya masafa hayo.

Akihojiwa na Radio ya Umoja wa Mataifa, mjumbe kutoka Tanzania, Innocent Mungy ambaye ni Meneja mawasiliano wa Tume ya mawasiliano nchini humo ametolea mfano masafa kwa ajili ya ndege zisizo na rubani, Drones..

(Sauti ya Mungy)

Amesema licha ya kwamba teknolojia hiyo bado haijashamiri sana Afrika lakini inaweza kuwa na manufaa kwa kuwa..

(Sauti ya Mungy)