Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Waandishi walindwe Bangladesh: Zeid

Waandishi walindwe Bangladesh: Zeid

Kamishna  Mkuu wa haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa Zeid Ra’ad Al Hussein, leo amelaani vikali mashambulizi yanayoendelea dhidi ya wachapishaji wa vitabu na  blogs nchini Bangladesh na kutaka serikali kuchukua hatua za dharura.

Katika taarifa yake Kamishna Zeid amesisitiza serikali ya nchi hiyo kuchukua hatua madhubuti za kuhakikisha ulinzi kwa wale wote ambao wanatishiwa na watu wenye misimamo mikali walioko nchini Bangladesh.

Amesema takribani waandishi watano na watoa misaada ya kibinadamu wawili kutoka nje ya nchi wamuewawa mwaka huu huko Dhaka na matishio mengine ya mashambulizi yanaendelea kutoka kwa vikundi ambavyo vinaamini vina haki ya kulazimisha mitizamo yao kwa makusudi kupitia  mashambulizi.

Kamishana Zeid ameitaka serikali kutoruhusu vikundi vyenye misiamamo mikali kushika hatamu na kutoa wito wa kufikishwa katika mkono wa  sheria kwa watekelezaji wa vitendo hivyo .