Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Licha ya hatari zaidi, Afrika Mashariki imejipanga kukabili El-Nino: UNISDR

Licha ya hatari zaidi, Afrika Mashariki imejipanga kukabili El-Nino: UNISDR

Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na kupunguza madhara ya majanga UNISDR imesema Ukanda wa Afrika ya Mashariki umeanza kushuhudia mvua za El-Nino, lakini kiwango cha juu kabisa kinatarajiwa kutokea mwisho wa mwezi huu.

Hiyo ni kwa mujibu wa Julius Kabubi, mtalaam wa UNISDR – ofisi ya Afrika Mashariki, alipozungumza na idhaa hii leo akisema

(Sauti ya Bwana Kabubi)

Hata hivyo amesema tangu mwezi Agosti mwaka huu ambapo taarifa za El-Nino zilipatikana UNISDR imewezesha watalaam wa mifumo ya tahadhari kwenye nchi za ukanda huo ili kuimarisha mifumo ya tahadhari na usaidizi, majanga yakitokea.

Hivyo amesema utayarishaji wa serikali umeimarika

(Sauti ya Bwana Kabubi)