Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano Mkuu wa UNESCO waanza Paris, Afrika Mashariki kunufaika.

Mkutano Mkuu wa UNESCO waanza Paris, Afrika Mashariki kunufaika.

Mkutano mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu ,sayansi na utamaduni UNESCO unaojadili bajeti na maazimio kadhaa yaliyowekwa miaka miwili iliyopita , umeanza jana mjini Paris Ufaransa ambapo kwa siku ya kwanza suala la maandalizi ya kamisheni ya elimu limetamalaki mjadala.

Akiongea na idhaa kutoka mjni Paris mwakilishi wa Tanzania katika mkutano huo ambaye ni Katibu mtendaji wa tume ya taifa ya UNESCO chini humo Dk Moshi Kiminzi, amesema ukanda wa Afrika Mashariki unayo fursa ya kunufaika katika mambo mengi kupitia mijadala na maazimio yatakayofikiwa.

(SAUTI DK KIMINZI)

Mbali na bajeti na matumizi ya UNESCO, elimu, sayansi asilia, sayansi za jamii, utamaduni na urithi wa dunia pamoja na habari na mawasiliano yatajadiliwa.