Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mchango wa wabunge wasisitizwa katika kupambana na rushwa

Mchango wa wabunge wasisitizwa katika kupambana na rushwa

Mkutano wa ngazi ya juu kuhusu ubia katika kupambana na rushwa umepongeza kujitoa kwa muungano wa kimataifa wa wabunge dhidi ya rushwa kwa mchango wake katika vita dhidi ya rushwa.

Katika mkutano huo uliofanyika leo pembezoni mwa mkutano wa sita wa nchi wanachama wa mkataba dhidi ya rushwa, COSP6, Mkurugenzi Mtendaji wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kudhibiti Madawa na Uhalifu, Yury Fedotov, amesema kuwa ofisi yake kama mlinzi wa mktaba dhidi ya rushwa, itaendelea kujitoa kushirikiana na wadau wote katika vita dhidi ya rushwa.

Bwana Fedotov amewaambia washiriki wa mkutano huo kuwa kuendeleza ubia ni muhimu hasa katika kufanikisha ajenda mpya ya maendeleo endelevu ya 2030.