Skip to main content

Tanzania yapata Makamu wa Rais mwanamke

Tanzania yapata Makamu wa Rais mwanamke

Tanzania imepata Makamu wa Rais wa kwanza mwanamke tangu nchi hiyo ipate uhuru mwaka 1961 na si mwingine bali Samia Hassan Suluhu, ambaye pamoja na Rais John Magufuli wataongoza serikali ya awamu ya Tano kwenye nchi hiyo ya Afrika Mashariki. Taarifa zaidi na Amina Hassan.

(Taarifa ya Amina)

Nats..

Samia Suluhu Hassan, akila kiapo jijini Dar es salaam, cha kuwa Makamu wa Rais wa Tanzania kufuatia ushindi waliopata akiwa mgombea mwenza wa Rais John Magufuli kupitia Chama Cha Mapinduzi kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 25 mwezi uliopita.

Bi. Samia kabla ya kuchaguliwa kuwa Makamu wa Rais, ameshika nyadhifa mbali mbali ikiwemo uwaziri na Makamu mwenyekiti wa Bunge la Katiba.

Umoja wa Mataifa nchini humo kupitia shirika lake la kushughulikia masuala ya wanawake, UN-Women lilikuwa mstari wa mbele kupitia mradi wa Wanawake Wanaweza, kuwajengea uwezo wanawake wagombea akiwemo Bi. Samia ambaye amemweleza Stephanie Raison wa shirika hilo kuwa mradi huo umezaa matunda kwa kuwa..

(Sauti ya Bi. Samia)

“Wamefanya mambo mengi kujenga uwezo wa wanawake wabunge na wawakilishi, kwa sababu awali mchango wao haukuwa mzuri sana bungeni na baraza la wawakilishi. Lakini sasa unaona michango yao imekuwa bora zaidi na unaona wamepata mafunzo mazuri.”