Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kufuatia ajali ya ndege Sudan Kusini, UNMISS yatoa usaidizi

Kufuatia ajali ya ndege Sudan Kusini, UNMISS yatoa usaidizi

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS unajiandaa kutuma usaidizi wake, ukiwemo walinda amani, kufuatia ajali ya ndege aina ya Antonov 12 iliyoanguka leo kwenye maeneo ya Juba nchini humo.

Taarifa hizo ni kwa mujibu wa  msemaji wa Umoja wa Mataifa Stéphane Dujarric alipozungumza na waandishi wa habari mjini New York Marekani,akiongeza kuwa ndege hiyo haikuwa ndege ya Umoja wa Mataifa wala haikusafirisha wafanyakazi wa Umoja huo lakini mamlaka za uwanja wa ndege wa Juba zimeiomba UNMISS kusaidia katika operesheni za uchunguzi na uokoaji wa abiria.

Halikadhalika Bwana Dujarric amesema kwamba UNMISS inatuma salamu zake za rambirambi kwa familia za wahanga na serikali ya Sudan Kusini.