Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kukosa baadhi ya takwimu ni kunyima watu haki zao: Mtaalamu

Kukosa baadhi ya takwimu ni kunyima watu haki zao: Mtaalamu

Kwa takribani wiki moja sasa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kupitia kamati zake limekuwa likipokea ripoti za wataalamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki mbali mbali duniani. Miongoni mwao ni ripoti kutoka kwa Mutuma Ruteere,

Mtaalamu wa haki za binadamu kuhusu ubaguzi wa zama za kisasa. Ripoti yake ilijikita zaidi katika masuala ya ukiukwaji wa haki za watu kwa misingi ya ukosefu wa takwimu zao katika ngazi ya kitaifa. Je nini umuhimu wa takwimu kwa misingi ya kabila na vikundi mbali mbali? Na je kwa nini baadhi ya nchi zinahofu kukusanya takwimu kwa misingi hiyo?

Assumpta Massoi wa Idhaa hii alizungumza na Bwana Ruteere mara baada ya kuwasilisha ripoti hii na hapa anaanza kwa kuelezea lile alilolipatia umuhimu zaidi kwenye ripoti yake.