Skip to main content

Mkuu wa UNRWA akutana na waziri mkuu wa Japan

Mkuu wa UNRWA akutana na waziri mkuu wa Japan

Kamishina Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA),Pierre Krähenbühl  amekutana na Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe na kubadilishana mawazo kuhusu ongozeko la mozozo Mashariki ya Kati na hatima ya wakimbizi wa Kipalestina.Taarifa kamili na John Kibego.

(Taarifa ya Kibego)

Miongoni mwa mengine yaliyojadiliwa katika mkutano wa kihistoria baina ya viongozi hao ni hatari ya kuibuka zaidi kwa vikundi vyenye misimamo mikali na mzozo wa wakimbizi unaosababishwa na mapigano nchini Syria.

Bwana Krähenbühl ambaye alisindikizwa na watoto wa Gaza kwelekea Japan, amesisitiza kuwa ni lazima dunia ikumbuke hatima ya wakimbizi wa Kipalestina wakati huu ambapo hali ya usalama inazidi kuzoroka Mashariki ya kati.

Aidha, ameipongeza serikali ya Japan kwa mchango wake tangu 1953 ambao umeiwezesha UUNRWA kuboresha na kupanua huduma za afya na kujenga miradi ya maendeleo kule Gaza na kutoa chakula na mahitaji mengine ya dharura kwa wakimbizi.