Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wakumbuka miaka 200 baada ya utumwa kukomeshwa

UM wakumbuka miaka 200 baada ya utumwa kukomeshwa

Baraza kuu la Umoja wa Mataifa leo limekuwa na majadiliano maalum kuhusu maadhimisho ya miaka 200 tangu kukomeshwa kwa biashara ya utumwa  kupitia bahari ya Atlantic. Amina Hassan na taarifa kamili.

(TAARIFA YA AMINA)

Majadiliano hayo yamejikita katika maudhui ya maadhimisho kwa mwaka huu ambayo ni wanawake na utumwa ambapo Rais wa baraza kuu Mogens Lykketoft amezungumzia umuhimu wa wanawake na wajibu wao katika jamii.

Bwana Lykketoft amesema licha ya kukomeshwa kwa biashara hiyo bado utumwa unaendelea na hivyo kuathiri wengi  hususani wanawake na watoto.

(SAUTI LYKKETOFT)

‘‘Chanagmoto kubwa inayotukabili leo ni kuchukua hatua mdhubuti kupinga kila aina ya ubaguzi ukiwamo wa rangi na wa kijinsia na kukomesha aina za utumw wa kisasa na udhihirisho wake ukiwamo wa kingono ambao huathiri zaidi wanawake na watoto.’’

Wazungumzaji wengine katika mjadala huo wamesisitiza umuhimu wa kukomesha utumwa unaoendelea hivi sasa huku wakisema safina ya marejeo iliyozinduliwa hivi karibuni mjini New York izidishe hamasa ya kupiga hatua dhidi ya utumwa.