Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sanaa yawezesha wakimbizi Kenya kujiinua kimaisha

Sanaa yawezesha wakimbizi Kenya kujiinua kimaisha

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR nchini Kenya leo limezindua maonyesho ya kazi za sanaa zilizotengenzwa na wakimbizi wanaoishi kambini nchini humo. Taarifa zaidi na Joshua Mmali.

(Taarifa ya Joshua)

Maonyesho hayo yamezinduliwa kwenye kituo cha utamaduni cha Ufaransa cha Alliance Francaise mjini Nairobi na faida zitokanazo na mauzo ya kazi hizo za sanaa zitanufaisha moja kwa moja wakimbizi waliozitengeneza.

Mradi huo uitwao Artists for Refugees umetekelezwa na UNHCR Kenya ambayo imewezesha wakimbizi wa kambi za Daadab na Kakuma nchini humo kujifunza sanaa kupitia warsha zilizoendeshwa na wasanii maarufu wakiwemo mwimbaji Henry Ohanga anayejulikana kwa jina la Octopizzo na mchoraji wa vikaragosi Victor Ndula.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo mkuu wa UNHCR nchini Kenya Raouf Mazou amesisitiza umuhimu wa sanaa katika kuelezea hisia za jamii akiahidi kwamba UNHCR itaendesha tukio kama hilo kila mwaka nchini humo.